Nyumba ya Rebecca Shaw ikiwa imevurugwa. Alipofika alifikiri kuwa ni damu iliyokuwa imetapakaa ukutani kabla ya kubaini kuwa zilikuwa 'tomato sauce'.

Polisi wakikagua ndani ya nyumba ya Rebecca ambapo Geraghty alisababisha hasara ya shilingi milioni 20.9.
 
Rebecca Shaw alikuta kila kitu kikiwa kimevurugika nyumbani kwake baada ya Geraghty kuvamia.
Kitanda cha Rebecca kikiwa kimevurugwa na kutupwa vioo.
Rebecca Shaw aliyevurugiwa nyumba na mpenzi wake aliyemkataa.
Gari la Rebecca ambalo nalo lilimwagiwa 'tomato sauce'.
Gari hilo likiwa limemwagiwa 'tomato sauce' kwa nyuma.
TV nayo ikiwa imeharibiwa na Geraghty.
MWANAUME mmoja aitwaye Martin Geraghty, 26, aliyekuwa na hasira za kuachwa aliamua kuvamia nyumbani kwa mpenzi wake Rebecca Shaw, 23, aliyekuwa na mimba yake huko Dover, Kent, Uingereza na kuvuruga nyumba yake na kusababisha hasara ya Paundi 8,000 sawa na Milioni 20.9 za Kitanzania baada ya kuambiwa na dada huyo kuwa hampendi tena.

Rebecca aliporudi nyumbani kwake alikuta vioo katika kitanda chake, mashuka yakiwa yamechanwa na nyumba yake ikiwa haitamaniki kwa uhalibifu uliofanywa na Martin aliyekuwa na hasira za kuachwa.

Martin alivunja vyombo na kuvitupa nje kupitia madirisha aliyoyavunja na kuharibu kila kitu alichokiona mbele yake pamoja na gari la Rebecca lililokuwa nje ya nyumba. Pia alivunja midoli ya mtoto wa Rebecca mwenye miaka minne na kurusha vyakula hovyo pamoja na 'tomato sauce' ukutani na sakafuni.

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top