Rapper huyo YMCMB ameigiza kama msaidizi wa Cameron. Kwenye filamu hiyo, Cameron anagundua kuwa kumbe yeye ni kimada tu kwa mchumba wake ambaye ameshaoa tayari.

Baada ya kugundua kuwa boyfriend wake ameoa, Cameron Diaz anajaribu kuyaweka sawa maisha yake yaliyoharibika. Lakini baada ya kukutana na mke wa mpenzi wake, anagundua kuwa wana mambo mengi wanayofanana na aliyekuwa adui yake huyo mkubwa anakuja kuwa rafiki yake kipenzi.
Lakini baada ya kugundua kuwa mpenzi wake ana mwanamke mwingine tena (wa tatu), wanawake wote hao watatu wanaungana kupanga kulipiza kisasi kwa mwanaume wao.
The Other Woman ni filamu ya vichekesho iliyoongozwa na Nick Cassavetes na kuandikwa na Melissa Stack.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top