Hivi karibuni Bongo5 ilizungumza na Mkuu Wa Vipaji na Biashara Mpya wa Rockstar 4000 / Sony Music Africa, Seven Mosha, ambaye aliahidi kuwa kazi mpya za Rose zitaanza kutoka mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni tarkribani miaka miwili toka muimbaji huyo asaini ‘record deal’ na label hiyo ya kimataifa.
Video ya Rose Muhando ‘Wololo’ pia imekuwa certified na mtandao wa video za muziki wa Marekani VEVO. Video hii imepandishwa youtube December 13 kupitia channel ya RoseMuhandoVEVO.