Baada ya Kijana Zitto kutangaza kesho kuwepo kwa mkutano na wahariri wa habari, waandishi wahaha kusaka vifaa vyenye ubora na kuchaji betri za camera ili kesho wapate kile walichokingojea.
Mitaani nako vijana wajiandaa kwenda katika mkutano huo, wengine wasema ni bora angeitisha mkutano wa hadhara moja kwa moja maana pale hotelini hawatapata nafasi nzuri ya kumshuhudia na kumpata moja kwa moja.
Lakini hii yote inaonyesha kuwa Zitto ni kivutio kikubwa sana kwa wananchi maana hata wanahabari wamehasika kusubiri kwa hamu siku ya kesho
Taarifa hapa chini imetolewa na ofsi ya mbunge ya zitto !!....
Mkutano na waandishi wa habari: Mhe Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo
Taarifa inatolewa kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari kesho siku ya Jumapili tarehe 24 Novemba 2013. Watatumia nafasi hii kutoa maoni na msimamo wao kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA ya hivi karibuni.
Mkutano huu na waandishi wa habari utafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kuanzia saa5.00 asubuhi.
Imetolewa na ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe, Dar es Salaam.
Jumamosi, 23 Novemba 2013.
Dar es Salaam