Leo Samsung wanaingiza madukani simu yao ya kwanza ya skrini iliyopinda kwa mtindo wa mbonyeo kutoka upande mmoja kwenda mwengine, ingawa Samsung sio simu ya kwanza kutoka na mpindo kwa vile Nexus zote sina sifa hiyo, lakini mpindo wa Galaxy Round ni mkubwa kulinganisha na Nexus. Nexus zote huwezi kuzijua kirahisi kama zimepinda mpaka auangalie kwa makini mno. Samsung Galaxy Round inaanza kuuzwa huko Korea ua Kusini siku ya leo.
Simu hiyo haina mambo maalum yanayoifanya iwe tofauti sana. Jambo pekee la aina yake ni kuwa unapoigusa upande mmoja wakati iko chini au mezani ambapo kwa vile imepinda hivyo inanyanyuka upande mmoja, hilo linapotokea Galaxy Round hutoa habari za muhimu kama vile simu ulizozikosa, saa, chaji ya betri na taarifa nyingine ambazo zinapatikana kwenye skrini wakati skrini imefungwa (lock screen)
Simu hiyo haitofautiani sana na Samsung Galaxy Note 3 kwa upande wa vielelezo ambapo inatumia prosesa aina ya Qualcomm Snapdragon 800 yenye kasi ya Quad-core 2.3 GHz, ina RAM GB tatu na kamera ya nyuma ina mp 13. Tofauti kubwa baina ya round na Galaxy Note 3 ni kuw anote ina S-Pen na Galaxy Round Round haina, Round ina pinda na ni nyembaba kuliko Galaxy Note kwa milimeta 0.4 ikiwa na upana wa milimeta 7.9. Pia Galaxy Round ni nyepesi kuliko Galaxy Note 3 kwa gramu 14 ikiwa na uzito wa gramu 154.
Nyuma Galaxy Round kama ilivyo Galaxy Note 3 ina gamba la ngozi lenye kuonyesha mishono ya nyuzi pembene, ambapo kwa maoni yetu gamba hili ni bora kuliko yale yaliyotangulia kwenye simu za Samsung ambayo ni ya plastiki. Kwa sasa simu hii itakuwa inapatika Korea ya Kusini peke yake ambapo Samsung haikutangaza ni lini simu hiyo itaingia katika soko la Marekani na Ulaya.
Kama ilivyo Note 3 Round pia ina skrini yenye ukubwa wa 5.7” ambapo inazifanya simu hizi ziwe katika kundi la Phablet. Hata hivyo wakati Betri ya Galaxy Note ina nguvu za kiasi cha 3200 mAh Round betri yake ni pungufu ikiwa na nguvu kiasi cha 2800, zote ni aina ya Li-Ion.
Endelea na takwimu za vielelezo hapo chini
Ingawa Simu hii ni ya aina yake kwa upande wa kupinga kwa skrini wengi miongoni mwa wateja wana hamu ya sifa mbili muhimu ambazo bado hazipatikani kwenye simu hii, sifa hizo ni kwamba wateja ni wenye kutarajia simu inayokunjika na sio tu iliyopinda na pia wengi miongoni mwa wateja wana hamu ya skrini ambazo hazivunjiki, ingawa Samsung tayari wanateknolojia ya aina hiyo kudizaini simu yenye sifa mbili hizi bado ni kitu kigumu, kwa vile wakati skrini inaweza kupinga vitu vingine kwenye simu havipindi. Na pia wakti flexible screen hazivunjiki pia hazina umadhubuti wa kutosha wa kutengeneza bila ya kuwekea kioo cha aina fulani, hivyo matumaini ya kupata simu zenye sifa mbili bado yako mbali.