Kushoto ni Zuckerberg Mwanasheria, kulia Zuckerberg “Toddler CEO” wa Facebook |
Hata hivyo akaunti iliyofutwa si ya Zuckerberg anayemiliki Facebook. Sakata hilo lililotokea wiki hii limetokana na kuchanganyikiwa kwa wasimamizi wa Facebook kwa kudhani Mark S. Zuckerberg mwanasheria maarufu wa Indianapolis anaiga jina la bosi wao. Facebook baadae wamegundua kosa lao hivyo kumuomba radhi mwanasheria huyo ambaye ni wakili anayetetea watu na makampuni yaliyofilisika. Facebook imo mbioni kuirejesha akaunti hiyo.
Zuckerberg
mwanasheria si mshabiki sana wa Facebook, lakini ametumia tukio hili
kujitangaza na kujiongezea umaarufu, Zuckerberg anatarajia kwamba
umaarufu huo utamfungulia soko jipya na kupata wateja zaidi. Mwanasheria
huyo amefungua website yenye anuani iammarkzuckerberg.com akiwaelezea watu kwamba naye ni mwenye jina hilo.
Zuckerberg
huyu anadai yeye haipendi Faceook kwa vile imesababisha kuvunjika kwa
ndoa yake lakini yupo humo kwa vile anatangaza biashara yake tu. Pia
amedai kuwa Facebook imemsababishia matatizo mengi ikiwa ni pamoja na
kusumbuliwa na watu wanaompigia simu wakiomba kutatuliwa matatizo ya
Facebook au msaada wa kufanya mambo fulani mbali mbali katika mtandao
huo.
Zuckerberg
mwanasheria anadai kwamba iwapo uli-gugul (google) Mark Zuckerberg
katika miaka ya 2004 au kabla basi hakika ulinipata mimi, lakini sasa
inabidi ugugul “Mark Zuckerberg Bankruptcy” kwa vile Zukerberg wa
facebook ni maarufu zaidi. Kama tulivyoeleza awali mwanasheria huyu
ametumia nafasi hii vizuri kwa kujitangaza.