Music Computing ni kampuni inayocheza na teknolojia, mbali na kutoa kompyuta yenye kasi ya ajabu na disk yenye ukubwa wa 21 TB, kampuni hii pia ina gajeti nyingine yenye kufurahisha, nayo ni Motion Command CT. Kwa jina unaweza ukadhani labda ni simulation ya ndege, kiuhakika hii ni meza ya kuweka ukumbini (sebuleni). Meza hii haiathiriki kwa maji (water proof) na ina skrini ya kompyuta, skrini hii inakuja na kompyuta ya Android. Pia inaweza kufanya kazi na OS za Windows 7 na 8 pamoja na Mac OSX. Pia inakuja na kompyuta ya Android.
Kwa mujibu wa Music Computing watengenezaji wa meza hii,  Motion Command CT ina skrini mguso (touch screen), hivyo unaweza ama kutumia Android moja kwa moja au kuiunganisha na tablet au laptop ya windows, na kwa upande wa Mac, kompyuta ya rahisi zaidi kuiunganisha itakuwa ni Mac Mini. Motion Command CT inaweza kuunganishwa na kompyuta mbili sambamba. Ingawa hazitafanya kazi kwa pamoja. Music Comptuing hawakueleza ni toleo gani la Android lililopo kwenye kompyuta yameza hii. 

Motion Command CT ina USB, Wifi (kama utaamua kutumia Android tu), na HDMI, kwa apps ambazo zimetengenezwa tayari kutumika na multi touch meza hii inakubali miguso mingi sambamba kwa wakati mmoja (multi touch) Rezolushani za Motion Command CT ni za HD kamili yaani 1920 x1080 (1080p). Pia inakuja na rimoti kwa ajili ya kuwasha na kuzima tu. 

Wakati skrini ina ukubwa wa 32” meza yenyewe ina ukubwa wa 46.5” na unaweza kuchagua rangi nyeusi au ya kahawia. Pia unaweza kuchagua skrini ndogo yaani yenye ukubwa wa 22”, na idadi ya juu kabisa ya miguso sambamba inayokubalika katika skrini hii ni 40. Kwa vile inahimili maji basi unaweza pia kunywea kahawa, au kinywaji chochote bila ya kuhofia kuiharibu.

Music Computing wanaeleza kuwa meza ya Motion Command CT imetengenezwa kwa umadhubuti maalum ambao unaruhusu meza hiyo kudumu kwa miaka kadhaa. Ili kuimiliki meza hii unatakiwa kuunguza jumla ya $ 3,300 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 3.34, ongeza na gharama za usafirishaji kutoka Marekani. 
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top