Jumuiya ya watanzania Washington Dc inasikitika kutangaza kifo mpendwa wao Zainab Buzohera Dullah au maarufu kwa jina la Zay B aliyefariki dunia saa mbili za usiku wa Jumamosi Januari 4 ,2014. Kwa mujibu wa mume wa marehemu Zainab alikutwa na umauti huko Doctors Community hospital Lanham Maryland baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu 5030 57th Ave Apt 303 Bladensburg Md 20710. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania inaendelea. Harambee itafanyika Jumapili January 5, 2014 saa 10 jioni katika anuani ifuatayo:5401 Annapolis Rd Bladensburg Md 20710.
Gharama ni $15, 000.
Tunakuomba tuma mchango wako kwenda CITI BANK. ATT: Ms. Ngalu Buzohera AC no.50070000.
Routing 9106834936
Shukran.