Boti
ya Kilimanjaro 2 iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa
dhoruba na kunusurika kuzama shuhuda ameongea na chumba cha habari
Clouds Fm na amesema boti hiyo ilipofika Nungwi ilizama mbele na
kunyanyuka nyuma,watu waliokuwa mbele wote wameachwa hapo hapo baharini
mpaka sasa manahodha wameendelea na safari kwa kuogopa kuzama endapo
wangesimama.
Boti
hiyo ina zaidi ya abiria 600,chanzo cha dhoruba hiyo kimeelezwa ni
upepo,kwa sasa abiria wamepewa life jacket kwa ajili ya kujiokoa,na boti
bado inaendelea na safari kuelekea Unguja,boti hiyo iliondoka sa 2
asubuhi Pemba.
Millardayo.com inaendelea kufatilia kwa undani taarifa hizi,endelea kuwa karibu.
Bonyeza play kusikiliza mashuhuda wakielezea Ajali hii.