MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya gari aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata mkubwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo na baada ya muda, wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina lake mbele ya jamii.
“Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.
Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.
Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”
“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?”
“Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia,” alisema Lulu