Hatua ya Baby Madaha kuwa msanii wa kwanza mwanamke nchini Tanzania, kujitokeza hadharani kumchambua msanii huyo mkubwa na mwenye heshma kubwa ndani na nje ya nchi, imevuta hisia za wadau wa muziki nchini huku akimwagiwa sifa kemkem kwa kujitokeza na kufuangua ufahamu wa wasichana kutokana na imani kwamba Diamond ni mchawi anayetumia nyota za wanawake kujipatia umaarufu.
Baby madaha ambaye anatarajia kuzindua Single nne pamoja na muvi yake kali zilizotengenezwa nje ya nchi, amesema kwamba kinachomkera zaidi ni kitendo cha Diamond kudhalilisha wasicha wenzake kimapenzi, kila kukicha kutoka na uwezo wake wa kifedha huku akitangaza wazi kwamba anafanya mapenzi bila kutumia kondom kwa madai kwamba anatafuta mtoto.
"Tarehe 22 Jumapili Disemba mwaka huu pale Golden Tulip nitamuonyesha Diamond,kuwa Queen of Swagg ni nani,ambapo yeye alizindua Single moja ya ngololo pale Serena mimi ninazindua single 4 moja ikiwa ni Soundtrack na Move yangu mpya ya the Galbladder, iliyonigarimu mamilioni kuitengeneza nje ya nchi,huku show nzima ikidhaminiwa na Heinekein ambao pia ndiyo wadhamini wa lebo ya Candy& candy ya jijini Nairobi, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa kiongozi mzito kutoka Ikulu ya Rais Kikwete pale Magogoni jijini Dar es Salaam"alisema Baby Madaha.
Kuhusu kauli yake kwamba Diamond ni mchawi alisema kwamba, "ingawa kuna maneno mengi kwamba Diamond ni mchawi na kwamba anaweza kuniroga, mimi hilo halinitishi kwa sababu yeye anashindana na wanawake badala ya kushindana na wanaume wenzake, katika maendeleo ila ukweli ni kwamba mimi si shindani na wanwake kwa sababu ni marafiki zangu, ila ninashindana na wanaume katika suala la maendeleo na siamini katika uchawi na akiona kwamba anaweza kuniroga kama ambavyo watu wake wananitangazia ajaribu,kwani mimi ninazungukwa na nguvu za Mungu na si Nguvu na Mganga wa kienyeji".
Baby Madaha alisema kwamba baada ya kumwangusha nyota huyo wa muziki nchini na kumfanya afikirie kumroga katika uzinduzi huo ataanza kufanya ziara nchini nzima kuitangaza Queen of Swagg itakayozidi kuipoteza ngololo ya Diamond katika ramani ya muziki ndani na nje ya nchi, kabla ya kuendelea na show kali sehemu mbalimbali Dunaini kama ilivyo pangwa na wanadhamini wkake wakuu Heinekein.