Juzi na jana kulikuwa na habari katika gazeti na mitandao mingi kuwa Wastara na Bond Bin Suleiman ni wapenzi na wamekuwa wakifanya siri sana huo uhusiano wao. Habari ambazo zilinukuu chanzo kimoja zilieanda mbali zaidi zikisema huenda Bond ana tabia ya kufanya mapenzi na mwanamke kotekote kwani aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Lulu Semagongo(Anti Lulu) alidaiwa kuwahi kukaririwa akisema kuwa anapenda sana kufanya mapenzi kinyume na maumbile na hawezi kuacha tabia hiyo. 

Baada ya habari hizo kusambaa ilibidi blog yetu  kuwatafuta mastaa hao wawili na wa kwanza kupatikana alikuwa ni Wastara na alikana kuwa katika penzi na Bond ila alisema wanafanya kazi pamoja kwani kwasasa wanashuti filamu mpya ya Bond inaitwa Uaminifu Dhaifu. Aliongeza kwa kusema kuwa Bond ni kama kaka yake. "sina mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na zile picha zote ambazo unaziona ni wakati tupo location tukiandaa filamu yake inaitwa Uaminifu Dhaifu, huo ndiyo ukweli, bora mume wangu angekuwepo haya yote yasingetokea.

Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bond ambaye yupo location wakimalizia filamu hiyo na alipoelezewa hayo alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Wastara na picha zinazodaiwa kuwa ni wapenzi ni za filamu mpya ambayo tuliweka hata hapa katika blog yetu, alisema kuwa huyo Anti Lulu anatafuta kuandikwa tu kwenye magazeti ndiyo maana anatoa habari hizo zisizo za kweli ili kujipatia umaarufu "Sio kweli ni picha za kazi tu ambazo hata wewe nilikutumia magazeti yanazigeuza, Lulu achana nae anatafuta kuandikwa, tulishachana kitambo wala hatuna mawasiliano.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top