Katika hali isiyokuwa ya kawaida na ya kushangaza, kumemezuka tabia ya vijana ambao wanashinda kakika kivuko kinacho unganisha Posta na Kigamboni wakivizia kivuko hicho kinapopita kupanda na baadae kinapo ondoka hata kikifika umbali mrefu wao kuanza kuruka na kupiga mbizi.
Mtandao huu wa Dar es salaam yetu umekuwa ukifuatilia kwa kina swala hili na kigundua kuwa hakuna mtu ambaye anawazuia vijana hawa wanaofanya mchezo wa hatari, ingawa kwa upande wa pili kimekuwa ni kivutio kikubwa kwa wale wasafiri..
Vijana hawa ambao hawalipii hata kiasi kidogo katika kivuko hicho wameendelea kuhatarisha maisha yao na pindi wakijua na kufahamu kabisa eneo ambalo kivuko kinapita huwa ni sehemu ndefu sana ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa kwao na pengine kifo.
Hata hivyo inawezekana wahusika hawalijui hili au lah wanalijua lakini hawalizuii, hili ni jambo letu sote kujiuliza.
Tazama sasa hapa kinacho tokea..... 
 Pichani ni Kijana ambaye alionekana anaruka kutoka Juu ya Pantoni(Kivuko) Mbele kidogo baada ya Pantoni hiyo MV. Magogoni kuanza safari zake, huku abiria wangi wakiwa wameacha viti vyao na kuendelea kushangaa.
 Wakati huo huo Kijana mwengine nae alionekana anachomokea kutoka katika Pantoni hiyo na kuzamia majini


 Wasafiri walipigwa Butwaa zaidi kuona kasi ya vijana hao inazidi kuongezeka na huyu kijanda ndiye aliyekuwa anafunga dimba la kuzamia majini.
 Hapa ni Baada ya vijana hao kuzamia majini na wengine hawaonekani yanaonekana maji tuu yanaruka wakati wao wapo chini ya maji hayo.
Ni zaidi ya Vijana 9 ambao wote walipanda Pantoni hiyo ya MV.MAGOGONI bila ulinzi wowote na baadae kupiga Mbizi wakitokea katika Pantoni hilo... 
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top