Zitto na Dk Mkumbo wanatuhumiwa kupokea fedha na kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuiua Chadema.
Ripoti hiyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kuandaliwa na Kitengo cha Upelelezi cha Chadema kwa ajili ya kufuatalia mwenendo wa Zitto kuanzia mwaka 2008.
Katibu Mwenezi wa Chadema, John Mnyika ameikana ripoti hiyo na kueleza kuwa haijaandaliwa na makao makuu ya Chadema.
Mnyika amebainisha kwamba Zitto ameibua jambo ambalo anafahamu kuwa limeshughulikiwa na uongozi wa cha hicho.
"Zitto anajua kuwa Andrea Cordes aliniandikia barua pepe na nakala kwake, nikawajibu kwamba ripoti hiyo hajaandikwa na makao makuu ya chama na tukipokea malalamiko rasmi tutachunguza kwa sasa chama kinachukulia ripoti hiyo kama ripoti nyingine zinazosambazwa mitandaoni," amesema Mnyika.
Soma hapa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Zitto ameutaka uongozi wa Chadema kutoa maelezi kuhusu taarifa iliyosambazwa mitandani kwamba anaivuruga Chadema.