Huu ni waraka wangu kwako wewe mdada ninaekupaga lifti asubuhi. Nimevumilia sana mpaka nimechoka aisee maana imekua ni kero sana. Toka tuanze biashara ya kupeana lift imekua tatizo sana mpaka najuta kukufahamu. Sina uhakika sana kama wewe ni member humu Jf,
But hata kama sio member, najua hukosi kufanya kazi na Member wa humu ambae sina shaka atakufikishia ujumbe.

1) Kwanza kabisa mimi ni mume wa mtu. Biashara ya wewe mke wa mtu kunipigiaga simu asubuhi asubuhi na kuniamsha siitaki. Mimi ninaamka kwa ratiba zangu, simu unazinipigiaga kuniamsha hua zinanipa wakati mgumu sana kujitetea kwa my wife wangu.

2) Sipendi kabisa tabia ya mimi kukusubiri wewe getini kwako. Mimi sio dereva wako, hujaniajiri wala kwa lifti ninayokupa sifaidiki chochote zaidi ya kua tu wewe ni jirani yangu, nakuonea huruma ukigombea daladala asubuhi. Wewe unatakiwa uwe umeshajiandaa asubuhi na nikukute getini. Cha ajabu siku hizi nikishafika getini mpaka nikupigie simu ndio utoke. Jana umeniuzi sana eti ulishajiandaa ila ukawa unasubiri nikupigie simu.


3) Kunichagulia nyimbo za kusikiliza kwenye gari sipendi. Mimi ni mpenzi mkubwa wa Bongo Flava, hizo R&B zako kama unazipenda sana basi ka-dowload ukasikilize nyumbani kwako/kwenu.

4) Inaendana na namba (3) pale juu. Hua napenda sana kusikiliza Magazeti redioni asubuhi. Sipendi kabisa tabia ya wewe kujifanya ndio controller wa radio ya gari langu. Kupitia Magazeti radioni ndio najua mambo mbalimbali yahusuyo Siasa, Mchezo n.k. kabla sijafungua JF.

5) Mimi sio mpenzi sana wa AC kwenye gari, napendelea kitu Natural Air. Sijui kwanini hujalifahamu hili. Eti ukiingia tu unaanza kupandisha Vioo na kuwasha AC, huangalii kama kio changu pia kimepanda ama vipi. Wewe unatakiwa unifuatishe mimi na sio kujifanyia mambo utakavyo.

6) Kuna mafuta mengine unapaka yananikera kwelikweli harufu yake. Nafikiri hata huko kazini kwenu wanaipata fresh.

7) Unaongea mno aisee, yaani kama umemeza kanda. Yaani njia nzima unaongea wewe tu. Binadamu tumepewa mdomo mmoja na masikioo mawili ili tuongee kidogo lakini tusikilize sana, lakini kwa wewe mdada sio hivyo aisee. Unahdithia mastory ya kazini kwenu ambayo hayanihusu, mi ya nini?? 

8) Ukiwa na mimi ujue ni straight to Mjini. Mambo ya kuniambia eti tupitie sijui Steers au Jamaa fast Food kuchukua vitafunwa mi siiizimkii aisee. Pengine wewe umezoea kuchelewa kazini, basi tusicheleweshane. Sometimes nakua na viporo kibao kazini nahitaji kuwahi kuvimalizia, we unaanza kuzusha safari zako za asubuhi asubuhi, why we mwanamke??

9) Hivi gari umejifunzia wapi?? Sijawahi kukuona ukiendesha na wala hujawahi kunionyesha hata leseni yako, leo unaniambia siku moja moja niwe nakuachia uwe unaendesha wewe, ili iweje?? Unataka kujifunzia gari kwangu? 

10) Mimi ndio dereva, najua wapi ni-over take na wapi nipite wapi. Cha ajabu hata speed unanipangia wapi nikimbize na wapi niendeshe slow, wewe umeomba lifti tu, kaa subiri ufikishwe kazini kwako, biashara ya njiani naijua mimi. Mimi nimeanza kuendesha gari toka unasoma shule ya msingi so sipendi ujifanye mwalimu wangu wakati naeendesha.

11) Gari yangu sio saluni kwenu. Eti unaweka miguu juu, mara sijui unakata kucha, halafu hizo kucha zinaporukia wala hujishughulishi kuzitafuta. Matokeo yake tunataka kuvunjiana ndoa. Halafu ukifungua kioo cha kujiangalia cha "kizuia jua" uwe unakirudishia baada ya kukitumia. Pia sipendi ukae kwa kulaza siti kwa nyuma. We asubuhi asubuhi umeamka bado una energy za kutosha halafu unakaa kwa kulaza siti, hizo kazi zitafanyika kweli??

12) Tena sipendi uwe unaongea kwa kunipiga piga begani au mkononi, hua naumia na pia naweza kupoteza control ya sterling. 

Haya ni baadhi tu ya ambayo unayafanyaga wewe abiria wangu naekupaga lifti ambayo yananikera sana asubuhi. Nashindwa tu kujua nianzie wapi kukuambia ukweli navyokereka.

Chanzo:Jamii Forums 
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top