Wanawake wa siku hizi wana tabia sawasawa na wanaume kasoro tu hawawezi kubadili jinsia ili wote tukojoe tumesimama...
Ukicheat na yeye anatafuta wa kwake anakomoa...Usipompa hela anatafuta danga linampa hela utashangaa tu wewe unafanya kazi una Nokia Asha,yeye anasoma Diploma ya Record Management pale Magogoni na babake ni Mchuuzi wa Samaki Feri lakini ana Samsung Galaxy Note3 mpya na kumuuliza huwezi...Ukidhani unamtumia kama Kipoozeo chake kumbe mwenzio na yeye anakutumia wewe kama Feni yake Joto likiwa kali..Ngoma Droo...We unalewa Bia ye anajidunga Shots za Tequila...Na mademu wa namna hii huwezi kusikia eti Baby nna mimba yako,hawapatagi mimba hawa hata ule rosti miaka 8,ukimwaga ugali wanamwaga mboga...wanaopata mimba hawa ujue wamekuja mjini na mbio za Mwenge...
Kuwa makini sana,Mapenzi ya siku hizi ni Timing za kumchinja Kobe,ukidhani umewahi kumbe umewahiwa,True Love ni ngumu sana kupata kama kusikia kolabo ya Suma Mnazaleti na Justin Bieber inapigwa chati za Billboard...
Kwa Hisani ya Mwanaume aliyeko dimbwini na Binti wa Kichaga
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top