Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu Johari atimkie Canada kumfuata mpenzi wake, Lulu Michael naye ameanza kujipendekeza kwa msanii Maarufu Justine Bieber kiasi cha kudiriki kumtongoza mtandaoni...
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Lulu Michael amekuwa akieleza jinsi anavyokosa usingizi kwa sababu ya dume hilo, hali inayomfanya akonde na kukongoroka.
Pamoja na maneno mazuri ya kumtongoza mwanaume huyo, tweet za Lulu zimeonekana kutokuwa na msaada wowote kwake kutokana na ukweli kuwa Justine Bieber ni mtu ambaye hajui kiswahili...
Mbali na kutoijua lugha ya kiswahili, Bieber ni mtu mwenye followers wengi sana ( 47,180,637 followers ), hivyo ni ngumu sana kutambua kwamba kuna mtu anayeitwa Lulu Michael.