hio picha hapo juu ni ya galaxy s4 fake ya kichina
hebu tuangalie specificatio za galaxy s4 ya kichina na original.
specification za galaxy s4 original
Processor: Quadcore snapdragon 600 1.9 ghz
RAM: 2gb
Kioo: inch 5
OS version: Android jelly bean 4.22
Hio hapo chini ni Original
Specification za galaxy s4 ya kichina
Processor: mediatek 1ghz quadcore
RAM: 1gb
Kioo: 5inch
OS version: Android jellybean 4.22
So nawatahadharisha wabongo kuwa makini na simu za bei rahisi na kujiona wamepata simu kali kwa bei rahisi.vitu vifuatavyo ufanye kuitambua simu hizi za kichina.
1. Camera Quality: Hata ikija na camera 13mp simu ya kichina itatoa picha vibaya hakikisha unapiga picha mbili tatu kujua quality
2. Download application yoyote ya benchmark, antutu ni nzuri pima score za simu yako kwenye proccessor, gpu na jinsi inavyo-render graphic kujua kama itascore kama galaxy original. score original zipo kibao online.
3. Charger yake usb na earphone hazina quality ya flagship
Je, zinafaa kununua?
Sio mbaya kununua hizi clone za kichina lakini hazi-deserve kuuzwa hela nyingi. Simu kama hii yenye quadcore 1ghz ina-deserve around 300,000 hadi 400,000!