Sonara
wa Liverpool, Uingereza Stuart Hughes ametengeneza iPhone 5 ya dhahabu
na almasi halisi,
yaani sio tu ya kuchovya. Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa Stuart Hughes
gamba
zima la simu hiyo ni la dhahabu ya kareti 24 na logo ya Apple, kifungo
cha
mbele cha simu na mzunguko mzima wa simu umewekwa vipande vya almasi ya
nyeusi ya kareti 26. iPhone hiyo unauzwa kwa jumla ya paundi za
Uingereza milioni kumi
sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 24.8
Sonara
huyu ambaye
hutengeneza gajeti, samani, mapambo ya gari, mapambo ya nyumba, mapambo
ya boti na vifaa vyengine na
kuvifanya viwe vya anasa na bei ya hali ya juu kwa ajili ya matajiri wa
Dunia.
Bila ya shaka yoyote kwa bei hii iPhone 5 hii ndio inakuwa simu ya ghali
kuliko
zote Duniani. Kwa mujibu wa maelezo ya Stuart Hughes imechukua jumla ya
wiki tisa kuitengeneza simu hii. Simu hiyo imepewa jina la iPhone 5
Black
Diamond yaani iPhone 5 ya almasi nyeusi.
Simu hiyo imebaki ikiwa na
maumbile halisi la iPhone 5 ambapo kifungo cha nyumbani (home button)
kimetengenezwa kwa almasi kiasi cha circa 600, ambazo zimelaziwa kwa
maji ya dhahabu kabla ya kukauka kwake. Nembo ya Apple imewekewa jumla ya
vipande vya alamasi 53. Jumla ya dhahabu iliyowekwa kwenye simu hiyo ina uzito
wa gramu 153. Na aina ya almasi iliyotumika ni almasi nyeusi.