SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa amerejea Jangwani.
Ikulu; Ngassa akiwa katika nyumba yake ya Mwanza. Hii ndiyo nyumba bora zaidi kati ya zote na itakuwa maskani yake akistaafu soka. Ipo eneo la Bwiru.
Hakuna maslahi makubwa aliyopata 


 
alikuwa anatafuta njia ya kutokea katika soka ya Tanzania na tangu Yanga SC hadi sasa unaweza kusema Mrisho ametumia kipindi hicho kuchanga vyema karata zake. Anamiliki nyumba tano, tatu zipo Mwanza na mbili Dar es Salaam- na ana gari nane, wakati huo huo akaunti yake wakati wote ikiwa ‘imefulia sana’ ina Sh. Milioni 20. Akiwa bado anategemea soka kama ajira yake, Ngassa amekwishaanza kujipanga kwa maisha ya baada ya soka na katika mahojiano na BIN ZUBEIRY anasema anafanya biashara ya usafirishaji kilimo.


 
Ngassa akiwa na Bibi na Babu
“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya shughuli za nyumbani wakati wote na mbili nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”. Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.    “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa sitegemei kurudi shule kusomea chochote, nitafanya biashara. Nimekwishaanza kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”. “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na siku moja nitatatambulika kama mwanasoka wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, tayari nina mashamba kama matatu, hapo nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  biashara kubwa,”anasema Ngassa. 
 
Ngassa akiwa na watoto wake
  Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili, ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora, ili wakue vizuri.
 
 Nyumba nyingine ya Mwanza
 
Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska nyota Tanzania. 

 
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.
 
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu

  Ngassa akiwa na watoto
   
Gari la Ngassa la Mwanzaa
 
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top