Menina Atick.
Akizungumza hivi karibuni Menina ambaye sasa anasumbua na
wimbo wake wa Shaghala Baghala alisema anachoamini ni kwamba msanii wa
kike mwenye kipaji hata asipotoa rushwa ya ngono, nafasi ya kung’ara
anayo, hivyo yeye atakuwa mfano kwa wengine.“Mimi…nitoe rushwa ya ngono ili nitoke, mh…kwa kweli hiyo haiwezekani, najiamini na sitakubali kuutumia mwili wangu kwa kugawa penzi ili nisimame kwenye muziki, kwanza nitatembea na wangapi,” alihoji msanii huyo.