Hivi karibuni Mariah Carey alizikonga nyoyo za mashabiki huko Angola kwa show ya maana iliyomuingizia kiasi cha dola za Marekani Milioni 1, sawa na bilioni 1 na milioni 600 za kitanzania.

Kundi la kutetea haki za binadamu ‘Human Right Foundation’ limemkosoa vikali mwimbaji huyo kwa madai kuwa alikubali kulipwa fedha na binti wa rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos, rais ambaye anatuhumiwa na baadhi ya makundi ya kutetea haki za binadamu kuwa fisadi.
Mariah Carey alipiga show ya masaa mawili nchini Angola iliyoandaliwa na Red Cross ya nchini humo, na kampuni ya simu ya Unitel ambayo inamilikiwa na binti wa rais Dos Santos aitwae Isabel.  Pia Isabel ndiye rais wa Red Cross nchini Angola.
Rais wa Human Right Foundation aitwae Thor Halvorssen ameandika tamko linalomkosoa Mariah Carey, “Mariah Carey haonekani kutosheka na pesa za dictator, imeripotiwa amelipwa dola milioni 1 kipindi hiki. Miaka mitano tu iliyopita aliperform kwenye familia ya dictator wa Libya Muammar Gaddafi.”

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top