MWANADADA anayetamba katika filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kero yake kubwa ni utumiaji wa simu za mkononi na anasumbuliwa sana na watu wasiokuwa na mambo ya msingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Lulu alisema simu zinasumbua sana na anatamani irudi enzi ya kutumiana barua posta.
“Sitaki kabisa kutumia simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua, yaani sijui hata nisimame wapi, kwani hata nikibadili namba ya simu inasambaa kwa kasi sana,” alidai Lulu.

Lulu alibainisha kuwa kwa siku anapigiwa simu zisizo na faida kwake na kwamba, idadi kubwa wanaompigia ni mashabiki wake, lakini wanakuwa na maneno yasiyo na msingi.
Kwa siku napigiwa simu nyingi sana ambazo ni kero kwangu. Nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu, nakubali kwamba wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa, ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu kwani ni sehemu ya kitendea kazi, aliongeza Lulu.


SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top