Kuelekea Christmas: Mtoto mwenye umri wa wiki mbili aweza kuigiza vizuri kuwa
Kuelekea sikukuu ya Christmas shamrashamra zinaendelea duniani ambapo waumini wa dini za kikristo wanafanya mambo mbalimbali kama ishara ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Ikiwa sehemu nyingi imezoeleka kutumia midoli kama ishara kuonesha jinsi ambavyo mtoto Yesu alivyokuwa amelala kwenye zizi la ng’ombe huku akizungukwa na mamajusi walioenda kumuangalia akiwa na mama yake Maria, huko Uingereza shule ya awali ya Dolphin katika eneo la Hove wamemtumia mtoto wa kweli mwenye umri wa wiki mbili tu kuigiza kuwa ‘Mtoto Yesu’.
Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Jessenia Henry aliwashangaza wengi kwa utulivu aliouonesha muda wote alipokuwa katika onesho hilo na hakuweza kulia hata kidogo, wakati ambapo anaigiza akiwa katika mazingira yaliyotengenezwa kama sehemu ya malisho ya wanyama.
Mtoto huyo alizingirwa na watoto 36 wenye umri kati ya miaka 3 hadi 4 walioigiza kama mamajusi.
Mkuu wa shule hiyo, Sheila Gavan amesema shule hiyo hujaribu kumtumia mtoto wa kweli na sio mdoli ili aigize na watoto wengine, na kwamba wazazi takribani 70 hualikwa kushuhudia igizo hilo.

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top