Kwa mujibu wa jarida  Bloomberg BusinessWeek, Bieber aliifuata kampuni hiyo mwaka 2007 (kipindi ambacho hakuwa maarufu) na kuwaomba awe balozi wao (brand ambassador).
Aliyekuwa Meneja Mkuu wa maendeleo ya biashara wa RIM alisimulia:
“Kitu kimoja tulichokikosa kilikuwa kwamba Justin Bieber alitaka kuwa mwakilishi wa BlackBerry. Alisema:  Nipeni $200,000 na simu 20 na ntakuwa balozi wenu. Tuliwapelekea wazo watu wa masoko na kuwaambia:  Huyu ni mtoto wa Canada, alikulia hapa, watoto watapenda.  
Walitufukuza na kusema ‘huyu mtoto ni wa muda. Hawezi kufika popote. Na mimi kwenye mkutano niliwaambia ‘huyu mtoto atadumu zaidi ya RIM.” Kila mmoja alicheka.
Of course, mwaka 2013 RIM walibadili jina na kuwa BlackBerry. Bieber … bado anaitwa Bieber.
Kipindi hicho kampuni ilikuwa hata haifanyi matangazo kwakuwa umaarufu wake kwenye biashara uliwapa kiburi kuwa watu wangenunua tu simu. Mambo yalianza kuwa magumu kwa Blackberry baada ya simu iPhone na zinazotumia mfumo wa Android kushika kasi.
Mwaka huu pekee, kampuni ya Blackberry imepoteza dola bilioni 1 kwa miezi mitatu pekee.  Kwa miaka mitano iliyopita, thamani ya kampuni hiyo imeshuka kwa asilimia 85 hadi kufikia dola bilioni 4  kutoka dola bilioni 80 mwaka 2008.
Mwaka 2013, kampuni ya Fairfax ilitoa ofa ya kuinunua BlackBerry kwa dola bilioni 4.7. Mwezi  September, kampuni ilitangaza kuwaachisha kazi wafanyakazi 4,500.
Wakati huo huo, Justin Bieber ameendelea kupeta. Kwa sasa ana utajiri wa $130million,na amekamata nafasi ya 9 ya Forbes ya mastaa wenye ushawishi zaidi duniani.
Pole yao Blackberry.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top