Umati wa wananchi waliokusanyika kumsikiliza Dk. Slaa leo mjini Kasulu Uwanja wa Kiganamo kabla ya mkutano kuvunjika.
Baadhi ya vijana waliokuwa na mabango wakati wa mkutano wa Dk. Slaa.
Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa uliofanyika Uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini leo umevunjika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi wakikabiliana na vijana waliorusha mawe kupinga mkutano usiendelee. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, vijana hao wanadaiwa kuwa kati ya 10-15 ambao walirusha mawe baada ya wananchi kuwafukuza wakitaka kuwapiga wakipinga kitendo chao cha kupiga kelele ili mkutano usiendelee ndipo polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na mkutano kuvunjika.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top