Wiki hii Nay wa Mitego alifanya mahojiano marefu na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto (Radio Citizen, Kenya) Willy M Tuva kuhusiana na mambo mengi kuanzia tofauti zake na Chidi Benz, Madee na Kimbunga. 


Nay wa Mitego akiwa na mtangazaji wa Radio Citizen, Willy M Tuva
Akijibu madai ya rapper Kimbunga kuwa alikuwa amepanga kumshirikisha kwenye hit yake Salam Zao lakini baadaye akamtosa, Nay alisema hakuwahi kumwambia kuwa angemshirikisha.
“Kimbunga ni mshkaji wangu, ni mtu ambaye hajielewi,” alisema Nay.

“Mimi sikuwahi kumwambia kwamba ‘nataka kufanya collabo na wewe’ hata siku moja. Lakini sijui alikaa na akina nani wakashikana masikio wakamwambia ‘bwana ukitaka kutoka pitia hapa’ akafanya hivyo. Mi sikuwa na time ya kujibizana naye, mimi niliendelea kufanya yangu. Siwezi kufanya competition na mtu ambaye hayupo level yangu.”

Akimuongelea Madee, Nay amesema kwanza hakubaliani na taarifa kuwa hitmaker huyo wa ‘Sio Mimi’ ni miongoni mwa wasanii wenye fedha nyingi.

“Ukisema Madee ni miongoni mwa wasanii ambao wanaingiza fedha nyingi sana hicho kitu hakina uhakika. Madee labda wimbo uliomuingizia hela ni ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’. Lakini ukitaja wasanii ambao wana hela Bongo, ukimweka Madee umekosea sana.” Hata hivyo Nay amesema ugomvi wake na Madee ni wa kibiashara na sio wa kupigana.

Akiongelea ugomvi wake na Chidi Benz, Nay alisema kwa sasa tofauti zao hazipo tena.
“Ziliisha tofauti zetu kama miezi mitatu hivi minne tulikuwa kwenye tour, tofauti ziliisha, yeye ndio alikuwa ana tofauti na mimi lakini mimi always sipendagi kuwa na tofauti na mtu ila nikiongea huwa naongea kitu cha ukweli. So this time tunaongea, tunapigiana simu kila kitu kiko sawa.”

SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top