Kwa kawaida kila binadamu anayop siri yake moyoni ambayo hapendi hata siku moja ifahamike. Lakini kwa upande wa wanaume haijalishi amekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda gani au amejuana na mwanamke kwa muda gani hiyo haiwezi kuwa ni kigezo cha kumuamini mpenzi wake kiasi cha kumweleza siri zake za moyoni. Kuna uwezekano zipo atakazoficha kwa muda lakini hapo baadaye akaamua kumweleza mwenzi wake, lakini kuna zile nyingine ambazo nitataja baadhi ambazo kamwe mwanamke asitarajie kuona mpenzi wake akifungua kinywa chake na kumweleza. Na hata ikitokea mwanamke akazijua kupitia kwa wapambe, ni dhahiri mwanaume huyo atakanusha kwa nguvu zake zote na hata aikibidi kutumia ubabe ili kuzima hoja hiyo..

Kwamba ana matatizo ya kifedha: Inawezekana wakati anakutana na mpenzi wake mambo yalikuwa safi na alikuwa na fedha za kutosha kula bata na kuishi maisha ya kifahari, lakini kama ikitokea mambo yakageuka ghafla bila ya kutarajia kwa mfano alikuwa na njia zake za panya za kupata fedha nje ya mshahara halafu njia hizo zikafungwa na mshahara ukawa hautoshi kabisa kukidhi hata robo ya mahitaji yake na mpenziwe, hapo mwanaume anaweza kutumia mbinu mbalimbali ili kuweka mambo sawa, ikiwezekana hata kukopa ili kusitiri aibu lakini si kumwambia mpenzi wake kwamba mambo yamegeuka, labda kama ni mkewe, lakini si mpenzi ambaye bado mambo hayajaiva

Kwamba aliwahi kubaka au kumla mtungo mwanamke na marafiki zake wakati fulani: Inawezekana historia yake ya ujana ilikuwa na vibweka vingi ikiwemo kubaka wanawake au kufanya mapenzi na mwanamke mmoja akishirikiana na marafiki zake vijana wa mjini huita mtungo au kula mande. Mwanamke asitarajie mwanaume atafungua mdomo wake na kuelezea huo upuuzi wake. 

Kukiri kwamba alikudanganganya ili akupate: Kuna wakati mwanaume hulazimika kudanganya au kuingia na gia kubwa kama vijana wa mjini wanavyosema ili kumpata mwanamke wa aina fulani. Kuna baadhi ya wanawake wamejiwekea viwango vya aina ya wanaume watakaopenda watoke nao, shida ni pale kina Bujibuji watakapokuwa wamefika bei lakini tatizo viwango viko chini, hapo ndipo mbinu na mikakati vitatumika ikiwezekana kujivika uhusika asiokuwa nao ili mradi ampate huyo mwanamke, na akimtia mikononi halafu mwanamke akashtukia kwamba ameingizwa Kingi na kujaribu kuhoji, asitarajie mwanaume huyo atakiri udhaifu. Lazima atajitahidi kutafuta namna ya kukwepa kuonekana muongo ili mradi kulinda hadhi yake ya uongo

Kukiri kwamba aliwahi kufungwa jela na kulawitiwa: Inawezekana mwanaume aliwahi kufungwa jela, lakini kama inavyojulikana misukosuko ya jela ni mingi ikiwemo kuingiliwa kinyume na maumbile, au inawezekana mwanaume katika mazingira fulani aliwahi kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kulazimishwa katika mazingira magumu na ya aibu. Kamwe mwanamke asitarajie kwamba mwanaume huyu atakuja kufungua mdomo wake na kumweleza mwanamke kuhusu jambo hilo. hata akija kulisikia mwanaume huyo atalipinga kwa nguvu zake zote. 

Mwanaume kukiri kwamba alikuwa ANASAFISHA KIWI CHA MACHO: Hata kama akikamatwa live na mpenzi wake akisafisha kiwi cha macho, si rahisi mwanaume akubali huo udhaifu, ni lazima atapinga kwa nguvu zake zote.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top