Wale wanaoifatilia Bongofleva kwa sana najua stori ya Mwana FA na Ay kuacha kufanya kazi na B Hits ya Hermy B mwaka 2012 sio ngeni kabisa ambapo ni stori ambayo wengi wa Watanzania waliona tayari ni beef na kila mtu kachukua zake, kitu kilichofanya pia Ay na Fa kuulizwa mara kwa mara kwamba wanabeef na B Hits.
Majibu ya maswali ya Watanzania yanaanza kupata majibu sasa ambapo usiku wa November 28 2013, Ambene (Ay) alipost hii picha hapa chini akiwa na Carol Ndosi, Arthur, Fid Q na Hermy B na kuandika hiyo msg kama unavyoiona hapo chini.
Hii ni ishara kwamba bado kuna muunganiko kati ya watu hawa japo ni muda sasa hivi hatujasikia single yoyote ya Ay imefanywa na B Hits.
B hits ndio ilihusika kutengeneza hits kadhaa za Ay na Fa kama ‘habari ndio hiyo’ ‘Nangoja ageuke’ na ‘Bado nipo nipo’