clip_image002[5]SNURA MUSHI
Na Hamida Hassan
STAA wa muziki wa Kibongo ambaye anatamba na kibao chake kinachojulikana kwa jina la Majanga, Snura Mushi, amefunguka na kusema kuwa akipata mwanaume anaachana na muziki.

clip_image002Madrasa aliyofungua Snura Mushi ikijulikana kwa jina la ‘Al Madrasat Miftahul Falah’.
clip_image002[7]Mkuu wa Madrasa alimtaja kwa jina moja la Mangale.
Mwanamuziki huyo ambaye pia ni muigizaji, hivi karibuni alimpeleka mwandishi wetu kwenye madrasa aliyofungua ambayo yeye ndiye anaihudumia ikiwa na watoto 120, ikijulikana kwa jina la ‘Al Madrasat Miftahul Falah’ iliyoko Kiwalani Kijiwe-Samri jijini Dar es Salaam na kumwambia kuwa ni shida tu ndiyo zinamfanya aimbe muziki.
clip_image002[9]Akizungumza na Championi, Snura ambaye amekuwa akiwavutia watu kutokana na uwezo mkubwa wa kukata mauno jukwaani alisema sababu kubwa ya kuamua kufungua madrasa hiyo ni kumshukuru Mungu na kuwasaidia watoto kupata elimu, huku akilipia kila kitu mwenyewe.
clip_image002[11]“Nimeona nimshukuru Mungu kwa njia hiyo ingawa bado simridhishi kutokana mambo ninayoyafanya, lakini kwa kunipa uwezo nimeamua kulifanya jambo hili kwa moyo kabisa kwani huwezi kuamini siku niliyozindua tuliandikisha watoto 70 na sasa tumefikisha watoto 120,” alisema Snura.
Je muziki na madrasa ni sahihi?
“Unajua pamoja na muziki mimi ni mtu ninayeijali sana dini yangu, hivyo kufungua kwangu chuo hicho si ndoto ya leo wala jana ni ya muda lakini sikuwa na uwezo. Sasa namshukuru Mungu nimepata uwezo wa kufanya hivyo.
Si kwamba anapenda kucheza muziki
“Usinione nacheka ninapokuwa jukwaani najitoa ufahamu ili nipate riziki, lakini kazi yangu siipendi kiukweli, kwani nakata mauno mbele za watu tu kwa sababu nataka mkono uende kinywani.
Je, akipata mwanaume itakuwaje?
“Nikipata mwanaume ambaye ataniwezesha kwa kunifungulia biashara ambayo itaniingizia fedha, hakika muziki kwangu utabaki kuwa historia, siupendi hata kidogo.
Vipi hajawahi kutokea wa hivyo?
“Ukweli hawa wote niliokutana nao wanataka kuniharibia maisha tu hakuna hata mmoja mkweli.
Kumbe amewahi kukutana na wanaume sita!
Mwenyewe huku akicheka anasema: “Nakumbuka katika maisha yangu yote nimewahi kukutana na wanaume sita, wote hakuna hata mmoja aliyenipa mapenzi ya kweli zaidi ya kuniumiza tu.”
CREDIT TO GPL
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top