DAH! inatisha sana..
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni
mfanyabishara wa magari kutoka jijini Mwanza,amemuua mwanamke mmoja na kujeruhi vibaya watu watatu kwa kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za
miili yao katika eneo la ilala jijini Dar es Salaam na kisha kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi.
Waandishi wa ITV walifika katika eneo la tukio ambalo lipo karibu kabisa na hoteli ya MM eneo la Ilala jijini Dar es Salaam na kushuhudia watu mbalimbali wakiwa wamezunguka eneo hilo huku gari aina ya Toyota Hilux Surf yenye namba za usajili T.537 iliyokuwa ikitumiwa na familia hiyo ikiwa imeharibiwa vibaya kwa kupigwa risasi huku damu zikienea ndani ya gari na maeneo mbalimbali ambapo baadhi ya mashuhuda wamesema.
Mkuu wa upepelezi kanda maalum ya Dar es Salaam kamishna msaidizi wa polisi Ahmed Msangi aliyewahi kufika katika eneo la tukio akiongozana na maafisa wengine wa jeshi la polisi, amesema aliyefanya mauji na kujeruhi watu watatu anaitwa Gabriel Munisi ambaye amedaiwa kuwa ni mfanyabishara wa magari kutoka jijini Mwanza, huku aliyeuawa kwa kupigwa risasi kichwani amejulikana kwa jina moja la Alfa,huku majeruhi wengine kama Francis Samwel ambaye alikuwa dereva wa gari iliyokutwa hapo amepigwa risasi kifuani,mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Hellen Elieza amepigwa risasi ya begani kulia kwa nyuma na Bi Christina Nando Newa anayedaiwa kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyabishara huyo aliyejiuwa alipigwa risasi ya paja.
Ndugu wa familia hiyo bwana Mloy Newa,amedai ndugu zake waliondoka na gari hilo hapo nyumbani kumsindikiza dada yao Bi Christina Nando Newa ambaye anadaiwa alikuwa akisafiri kwenda Saipraz na baadhi yao walikuwa wakienda makazini huku mkuu wa kitengo cha dharura kutoka hospitali ya amana dakta Christopha Mzava akithibitisha kupokea majeruhi na miili ya marehemu katika hospitali hiyo.