Halima Yahya ‘Davina’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kwamba anaichukulia ndoa yake kama chuo cha mafunzo kwa jinsi alivyobadilika na kuwa tofauti na Davina aliyekuwa nje ya ndoa.“Nimekuwa tofauti kabisa na Davina wa kabla ya ndoa, sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi,” alisema.
Akifafanua zaidi, Davina alisema zamani alikuwa ni mtu wa kurandaranda hovyo tofauti kabisa na hivi sasa.
“Zamani nilikuwa napenda safari zisizokuwa na faida tofauti na sasa hivi, kweli nimeamini ndoa ni chuo cha mafunzo,” alisema huku akiwaombea wasanii wenzake walio nje ya ndoa wafunge ndoa na kuwa na familia zao kwani watajifunza mengi.
-GPL