Msanii wa filamu Nchini Jaqueline Wolper amekuwa mstari wa mbele katika harambe mbalimbali hasa pale anapooalikwa na kudhuria katika matamasha yanayohusu wasanii na hata wale ambao si wasanii katika shughuli zao na kutoa michango ambayo yeye anasema ujisikia kutoa japo kuna watu wanaweza kuwa na fedha zaidi yake.
“Suala la kutoa kama tunavyoambia hata katika vitabu vya dini ni moyo wa utoaji kuna watu ambao wana fedha kuliko hata mimi lakini wanaweza kuwa wazito katika utoaji kwa ajili ya kuwasaidia wengine, lakini kwangu nikitoa najisikia amani katika moyo wangu,”anasema Wolper
Msanii huyo nyota katika tasnia ya filamu Bongo hivi karibuni alitoa ahadi ya milioni 2 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya watoto katika kanisa la KKKT- Kijitonyama, Wolper ndio alikuwa msanii pekee alimchangia mwigizaji mwenzake marehemu Sajuki milioni 16 ili akatibuwe nchini India