Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
Baby madaha ambaye hivi sasa yuko nchini Kenya kwa shuguli za muziki amesema kwamba, Diamond hajui kuimba na ndiyo maana amekuwa msanii wa matukio huku nyota yake ikiegemea kwenye mapenzi na wasichana wenye majina makubwa hususn wasanii.
Akizungumza na mpekuzi wetu katika mahojiano maalum leo baby Madaha alisema kwamba, “Binafsi niliposikia kwamba Diamond anaumiza kichwa kunasa penzi la msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) sikushangaa hata kidogo. kwa sababu nilitambua kwamba soko lake la muziki limeanza kushuka hivyo lazima atafute eneo lingine la kujiimarisha kibiashara, ili jina lake liendelee kuwika”.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza kuporomoka”alifafanua Baby Madaha.