Mwanamuziki Diamond Platnumz aka Rais wa Wasafi anaetamba kwa wimbo wake No. 1 haishi drama na warembo wa mujini.
Baada ya hivi karibui kuonekana na Wema na kuwapa fans wake na wa Wema matumaini kwamba wamerudiana ghafla ameibuka kupitia Global Publishers na kusema “Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond na kuendelea kusema “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”Maneno hayo yamewakera fans wa Wema aka #teamwema kupita kiasi wakiwemo [dougiemasta12, matikibokoyao na wengine wengi] ambao wametiririkia kupitia Instagram na kuonyesha hasira zao kwa kile wanacho dai kwamba Diamond hana adabu na anadhalilisha wanawake especially Wema wao.
Yaani hii #teamweam wako tayari na standby kumtetea Wema wao katika hali yeyote ile. Na ni kwamba wamejitolea muhanga kumsupport Wema 100%.
Haya ndo mambo yanayoendelea huko Instagram hebu jisomeeee mwenyewe....
Yaani comment ni nyingi sana unaweza ingia instagram ukajisomea. Wadau wana hasira sana na Rais wa wasafi ama kweli hawa ni 100% ride or die loyal fans wa Wema.