mtandao wa 1G
hii ndo network ya kwanza kabisa ilikua katika mfumo wa analog na ilitumika toka miaka ya 80 kwenye simu za zamani, ilikua slow na hata ubora wa sauti ulikua mdogo. mtandao huu ulitengenezwa kwa ajili ya sauti tu hapa watu walikua hawaingii internet kwa simu.
mtandao wa 2G
dunia ikaanza kuchangamka mtandao wa 2G ulipoingia kupiga simu kukawa kuzuri na sauti ikaongezeka ubora. hapa tukaanza kuona kitu kinaitwa edge na gprs na simu zinazotumia internet. japo internet ilikua slow lakini watu waliweza kuitumia kwa mambo madogo kama kuchat na kubrowse kurasa za website ambazo ni nyepesi. ukiona simu au kifaa chako cha internet kinakuandikia E au G ujue wewe bado upo zama za 2G
mtandao wa 3G
dunia ikazidi kuchangamka na sasa hivi Tanzania na East Africa kwa ujumla tupo kwenye 3G, hapa internet imezidi kuwa na kasi kiasi ambacho watu wanaweza kudownload na kusikiliza online video na miziki. watu wanawasiliana kwa video dunia nzima. tukaanza kuona na modem zilizofanya computer zetu ziweze kupata internet. ukiona simu yako au kifaa chako kinaandika 3G, h, h+, hspa, hsdpa, hsupa, wcdma au hspa+ ujue upo kwenye 3G.
mtandao wa 4G
hapa ndio tunakoelekea ila wenzetu ulaya na marekani tayari washaenda huku, internet yenye speed kubwa kiasi kwamba unafungua kurasa za tovuti kama vile zimehifadhiwa kwenye computer kumbe zipo online. ukiona kifaa chako kinaandika 4G au lte ujue upo katika ulimwengu huu.