Kampuni
ya Microsoft imeingia jikoni kuanza kupika software ambayo itatumiaka
kwa njia ya mtandao (remote network) kuingizwa katika tableti au
kompyuta. Huduma hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ni sehemu ya Windows miaka
ijayo imepewa jina la awali Microsoft Mohoro. Mohoro ni jina la mji uliopo kusini mashariki mwa kisiwa cha Ngazija (Comoro) karibu na mji wa Fumbuni.
Microsoft
Mohoro bado ipo katika hatua za awali ambapo kwa mujibu wa taarifa za
Business Insider, Mohoro itakuwa ndio njia mpya ya kutumia Windows ikiwa
kama huduma ya desktop, hii ina maana kwamba itaweza kuwekwa kwenye
kompyuta au tableti kwa njia ya mtandao kwa kutumia kompyuta nyingine,
kupitia Mohoro tableti na kompyuta zitaweza kuwekewa Windows kwa njia ya
beaming (kurushwa kwa kutumia internet)
Katika
hatua hizi za awali Microsoft bado hawakutoa taarifa rasmi ya huduma au
software hii, ambapo kwa taarifa za CNet imeelezwa kwamba huduma hii
itarajiwe kuwa tayari katikati ya mwaka 2014. Hii ina maana vifaa
visivyotumia Windows kama vile iPad au tableti za Android huenda
vitaweza kutumia OS hiyo katika mazingira ya virtual.
Mohoro
itakuwa ni jaribio la kwanza kabisa la Microsoft kufanya kitu cha namna
hii, ila inaaminika kuwa Microsoft watatoa taarifa zaidi kuhusu Mohoro
kwenye mkutano wa watengenezaji wa programu za Microsoft utakaofanyika
mwezi wa Tisa mwaka huu. Bila shaka jamaa zangu kutoka Mohoro, Moroni
hadi Mitsamiouli wataburudishwa na jina la programu hii. Ngarijo onana
maudu.