Akiwa
 na umri wa miaka 59, Mtangazaji hodari wa show za mahojiano duniani 
Oprah Winfrey ambae miezi kadhaa iliyopita aliitembelea Tanzania kwenye 
mbuga za wanyama, amesema hajutii kutokuwa na watoto maishani mwake.
Oprah
 ambae aliwahi kubakwa akiwa na umri wa miaka 14 na kujifungua mtoto 
ambae hata hivyo alifariki dunia siku chache baada ya kuzaliwa,  
anaamini kama angekuwa mama maisha yake ya kazi yangeingiliana na maisha
 yake ya familia .
Anakwambia
 ‘kama ningekuwa na watoto kwa hakika watoto hawa wangenichukia, 
wasingeweza kunipenda kwa kuwa wangeingia kwenye ushindani na kazi 
yangu, wangekuwa kama watu wengi mnaowaona kwenye show zangu 
wakizungumzia familia zao kutokuwa na mapenzi na watoto wao, maishani 
mwao wangekosa kitu muhimu ambacho ni upendo wa mama’

