Mimi ni kijana wa kitanzania, najitokeza hapa mbele yenu kuomba ushauri kwa haya makubwa yaliyonikuta.

Nilianza chuo miaka mitatu iliyopita, nikimaanisha kwa sasa nipo mwaka wangu wa mwisho katika hii kozi ninayoichukua. Nilianza chuo bila kuwa na uhusiano wowote ule wa kimapenzi na msichana hapa chuoni kwa mwaka wote ule wa kwanza.

Hali hiyo ilibadilika baada ya kuingia mwaka wa pili, kwani kipindi hicho kukawa na mwaka wa kwanza wanaingia na bahati nzuri nikatokea kumpenda msichana mmoja mrembo wastani sema ni mstaarabu haswaa. Nilijaribu bahati yangu na mungu si athumani huyu msichana akanikubalia na tukaanza mahusiano yeye akiwa mwaka wa kwanza,mimi wa pili. Tuliishi kwa amani na  furaha kwa kipindi chote kile(nikimaanisha semester zote mbili za mwaka wangu wa pili).

Kinachonifanya kuandika hapa ni hiki sasa, mwanzoni mwa semester iliyopita nilianza kusikia tetesi kutoka kwa marafiki zangu ya kuwa huyu msichana niliye naye anatoka na mmoja wa ma-lecturer wanaomfundisha. Sikuliamini hilo, nikaamua kumuliza mwenzangu kwamba nimesikia hili na hili, je kuna ukweli wowote? Alikataa kata kata na kusema huo sio ukweli na nisiamini kila ninalolisikia, kwa kuwa ni mstaarabu sana na kwa jinsi alivyokuwa akiongea basi nikamuelewa kwa muda ule.

Ila sikuishia hapo nikaendelea na uchunguzi wa chini chini bahati mbaya sikuambulia lolote kuhusu uhusiano wake na  huyo lecturer zaidi ya yeye kuwa na ratiba ya  kwenda kwao kila baada ya wiki mbili kuanzia ijumaa jioni mpaka jumapili ambao ni utaratibu wake toka anaanza chuo. Na hiyo ijumaa mpaka jumapili akiwa nyumbani mawasiliano yalikuwa yakipungua sana kwa sababu alikuwa akisema anakuwa busy sana na shughuli za nyumbani kwao na hata usiku ukimpigia simu alikuwa hapokei kwa madai analala na ndugu yake na kwahiyo atakuwa anampigia kelele.

Leo mchana sasa, nilimpigia simu twende tukapate chakula cha mchana lakini alikataa na kuniambia kuna kazi anaifanya kwanza mpaka aimalize ndio ataenda kula, mimi nikatangulia kwenda kula ila wakati narudi nikakutana na rafiki yangu, akaniuliza mbona nimekutana na bibie(mchumba wangu) anakula na Mr. X (huyo lecturer niliyeambiwa anatembea naye ) sehemu flani(ma-lecturer wengi ndio wanapokula hapo na kama utakuta wanafunzi basi ni mmoja mmoja ambao wako vizuri sana kifedha)… sikuamini, nikaenda kuhakikisha… Nilichokiona aisee sikuamini macho yangu, wote wawili walikuwa wamekaa wakipata lunch tena wakionekana wenye furaha.

Nilimpigia simu lakini hakupokea, aliishia kuiangalia tu simu yake na kuirudisha kwenye meza… Nikamtumia meseji ya kwamba nimemuona na nimezima simu yangu mpaka sasa, hapa natafakari nimfanyaje huyu msichana kwa hili alilonifanyia??? It hurts kwa kweli ikizingatiwa huyu lecturer ana mke kabisa so what if ndio tabia yake hiyo kutemebea na wanafunzi? Si  ndio kuambukizana magonjwa huku??

Naombeni ushauri wenu , nimfanyeje huyu kiumbe??

"LIKE HABARI HII HAPA CHINI"
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top