Didier Drogba and Emmanuel Eboue walimiliki headlines baada ya kuingia kwenye mikono ya kuadhibiwa kwa kitendo chao cha kuvaa na kuonyesha bila kibali maalum, nguo zenye maandishi ya kumuenzi Mzee Nelson Mandela.
Shirikisho la soka la Uturuki limeamua kuwasamehe wakali hawa ambaoo walikua waadhibiwe kwa kulipa faini kutokana na hicho kitendo walichokifanya baada ya game ya Ijumaa ya Galatasaray ambao walimuenzi Mandela kwa kuweka picha yake nje ya uwanja na kuandika Your legacy is in our hearts’.
Hata hivyo pamoja na hayo, Didier alionekana kama hajali ambacho kingetokea kwa kusema angefanya kitendo kama hicho tena na tena kumuenzi Mzee Madiba.