Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika tarehe 24/12/2013  katika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza.

Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone anatarajia kuwaburudisha wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkesha wa Christmas, December 24.
 
Ben ambaye ni moja kati ya mapromota waliomsainisha Chameleone mkataba wa kupiga show hiyo amewahakikishia wakazi wa jiji hilo kuwa show hiyo itakayofanyika eneo la ufukweni (Charcoal Ribs) itakuwa ya ubora wa hali ya juu.
 
"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika ufukwe wa Charcoal Ribs Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Amesema Ben.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO
 
Top