Kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini likishambulia jukwaa la Leaders Club kabla P-Square hawajapanda usiku huu.
Mwanamuziki Joseph Haule 'Profesa Jay' akiwapagawisha vilivyo mashabiki waliohudhuria shoo ya P-Square Live in Dar ndani ya Viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar.
Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee' au 'Anaconda' akiwapagawisha mashabiki wake waliohudhuria katika Viwanja vya Leaders Club usiku huu katika shoo wa wakali P-Square.
Mwanamuziki Ben Pol akiwasha moto katika steji ndani ya Viwanja vya Leaders usiku huu katika shoo ya P-Square Live in Dar.