Taarifa hiyo inaeleza kwamba mikakati hiyo inalengo la kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa, ambaye leo anaendelea na ziara yake Mkoani humo,tangu Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazi kuvuliwa madaraka yake ndani ya Chama hicho, kufuatia madai ya kupanga njama za kuung'oa uongozi uliopo madarakani akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Slaa.
Mikakati hiyo itafuatiwa na maandamano makubwa kueelekea eneo la mkutano, hii ni mara ya pili kwa mipango kama hiyo kufanyika baada ya ile ya jana kufanikiwa, ambapo mkutano wa Dkl Slaa ulivunjika huku Askari wa Jeshi la Polisi wakilazimika kutumia nguvu na kurusha mabomu ya machozi kuwatanya wanachama wanaopinga ziara hiyo mkoani humo.
Awali Uongozi wa Chadema Mkoa wa Kigoma ulitahadhalisha kuhusu ziara hiyo na kudai kwamba, hali si shwari katika mkoa huo kutokana na wanachama wa Chadema kuchoma Bendera na kubomoa mawe ya msingi katika ofisi mbalimbali za Chama hicho.
Wakati hayo yakiendelea Katibu Mkuu huyo (Dk Slaa) amekiri kuwepo kwa hali mbaya lakini akisisitiza kwamba, kamwe hawezi kukatisha ziara yake, mkoani humo na kama ikibidi kufa basi yuko tayari kufa, awali kabla ya vurugu hizo kuanza Habarimpya.com pia iliwai kuandika habari juu ya mikakati iliyopangwa na wanachama wa Chadema wanaopinga hatua ya Kamati Kuu ili kusoma habari hiyo bofya maandishi ya bluu.